Home » » Kylie Jenner mwenye umri wa miaka 20 adaiwa kuwa na ujauzito

Kylie Jenner mwenye umri wa miaka 20 adaiwa kuwa na ujauzito

Written By Bewith Jeddy on Saturday, October 14, 2017 | 2:43 PM

Imeripotiwa kuwa Kylie Jenner mwenye umri wa miaka 20 (mdogo wake na Kim Kardashian) ana ujauzito wa mpenzi wake (boyfriend) Travis Scott. Inasemekana ujauzito huo kwa sasa una miezi 5 na Kylie amemkodisha mtaalam wa waja wazito aje kumfanyia mazoezi na kumpangia chakula (lishe) anayotakiwa kula wakati huu wa ujauzito.

Kylie anasadikika kuwa ametengeneza USD Milion 41 kwa kipindi cha mwaka 2017 kutokana na mauzo ya bidhaa zake za urembo na reality show ya familia..
Pia inasemakana Dada yake Khloe Kardashian naye ana ujauzito wa mpenzi wake wa sasa ambaye anaitwa Tristan Thompson ambaye ni mchezaji wa Basketball (mpira wa Kikapu) nchini Marekani.
Inasemekana pia Kim Kardshian anatarajia kupata mtoto wa tatu kupitia njia ya Surrogation.

Mpaka sasa familia ya hao warembo haijajitokeza kukanusha chochote juu ilo.

TUNAWATAKIA KILA LA HERI.

0 comments :

Post a Comment