Home » » Toni Braxton, Birdman wageuka gumzo!

Toni Braxton, Birdman wageuka gumzo!

Written By Bewith Jeddy on Thursday, June 30, 2016 | 2:14 PM

STAA wa Muziki wa R&B, Toni Braxton na mkali wa Hip Hop, Birdman wanaodaiwa kuwa ni wapenzi hivi karibuni waligeuka gumzo ukumbini baada ya kuonekana wamegandana kwa muda mrefu.
Toni Braxton, BirdmanTukio hilo lilitokea katika sherehe za utoaji Tuzo za Black Entertainment Television (BET 2016) ambapo inasemekana wakati wanaingia ukumbini hapo walikuwa wameon-gozana pamoja huku wakishikana mikono kimahaba.
Wawili hao wameingia katika uhusiano wa kimapenzi mwezi uliopita ambapo kwa mujibu wa Jarida la People, Birdman amekuwa akikanusha kuwa na uhusiano na staa huyo japokuwa uongozi wa Toni umeweka wazi kuwa ni wapenzi.

Awali, Toni alikuwa ameolewa na Keri Lewis ambaye walizaa naye watoto wawili na mwaka 2013 walibw-agana.

0 comments :

Post a Comment