Home » » Snura ahofia ‘Chura’ kupotea!

Snura ahofia ‘Chura’ kupotea!

Written By Bewith Jeddy on Thursday, June 30, 2016 | 2:08 PM

STAA wa Muziki wa Mduara, Snura Mushi ‘Snura’ amefunguka kuwa hakuna kitu kinachomuogopesha kwa sasa kama kufanya ‘dayati’ kwani kutasababisha makalio yake ‘Chura’ kupotea.
Akizungumza na Amani, Snura alisema kuwa kuna kipindi aliwahi kujikondesha akapata shoo mikoani lakini cha ajabu kila alipopanda jukwaani mashabiki walikuwa wakipiga kelele kuwa wanamtaka Snura kwani waliyempandisha hakuwa yeye kutokana na Chura kuonekana mdogo.
 “Nachukia sana kufanya dayati maana inanipunguzia mashabiki kama nilivyoenda mikoani kipindi fulani kidogo nisha-mbuliwe na mashabiki kisa hawamuoni Chura waliyemzoea mwilini mwangu,” alisema Snura.
Hivi karibuni wimbo wa Chura wa msanii huyo, ulifungiwa na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kutokana na kukosa maadili.0 comments :

Post a Comment