Home » » Dinna Marios; nilipoteza kipindi kwasababu ya mtoto wangu

Dinna Marios; nilipoteza kipindi kwasababu ya mtoto wangu

Written By Bewith Jeddy on Sunday, February 21, 2016 | 8:45 PM

Nilipompata Zion kama mzazi yoyote ilikuwa ni furaha sanaa alileta furaha maishani mwangu na mwanzo mpya katika maisha yangu.

Katikati maisha yangu yoote nilikuwa muoga sanaa kupata mtoto sikuwa najua nitaanzia wapi kumlea.Zile story za wakinamama waliotangulia kuwa kuzaa kunauma zilikuwa zinanipa stress saana.

Lakini Nilimuomba Mungu nikifikisha miaka 30 Mungu anijaalie mtoto katika mahusiano yanayoeleweka.Zion hakuwa bahati mbaya siku ambayo baba yake alisema anatamani tupate mtoto Mungu aliweka tiki matamanio hayo wiki iliyofuata nilishika ujauzito.
Nikiwa natimiza miaka 30 nilikuwa na mimba kubwa ya Zion na nikamzaa nikiwa na miaka 30 nikaamini ni mpango wa Mungu.

Nilipopoteza leo tena nilihuzunika sana nikaanza kukufuru Mungu.Kwamba kwa miaka 8 mfululizo nimekilea kipindi leo nimeenda kujifungua narudi nakuta nafasi hiyo haipo kwa nini?kwa nini kuzaa kubadilishe tena ghafla?nakumbuka siku hiyo hata kunyonyesha sikuweza kabisa kabisa
Lakini nikamuomba Mungu anipe muongozo anataka kunipeleka wapi?Kwa sababu ya Zion niliweza kuja na product ya mafuta ya nazi dina marios coconut baby oil.
Alipotimiza mwaka mmoja picha za birthday yake ndio zilileta wazo la kuanzisha magazine ya parenting/malezi .Later nikajoin @efm_93.7 radio nakuanza kipindi kipya cha UHONDO.

Nilianza upya na MTOTO wangu Zion ndio inspiration ya mwanzo wangu mpya.Baada ya mwaka mmoja kupita wa kulipika wazo jana nikafanikiwa kutambulisha magazine ya MTOTO kwa ndugu,jamaa na marafiki waliokuja katika birthday party ya Zion.

Na magazine cover story toleo la kwanza yupo Zion na mimi mama yake kukusimulia mengi maana yeye ndio inspiration ya hiyo magazine.

Lolote tunalomuomba Mungu atatupa lakini sio kwa picha ile tunayoitaka ni kwa namna apendavyo yeye na anavyoona inakufaaa.

Usikose nakala ya MTOTO magazine kuanzia wiki ijayo kusoma mengi yahusuyo malezi ya watoto wetu . Litauzwa Tsh 5,000 tu!


0 comments :

Post a Comment