Home » » Yemi Alade atungiwa nyimbo ya kiswahili na Sauti Sol

Yemi Alade atungiwa nyimbo ya kiswahili na Sauti Sol

Written By Bewith Jeddy on Monday, January 18, 2016 | 9:02 AM

Staa wa muziki anayekimbiza Nigeria, Yemi Alade.

KAMA ulikuwa hujui hii inakuhusu! Staa wa muziki anayekimbiza Nigeria, Yemi Alade amemuanika aliyefanikisha Wimbo wake wa No Gode kuimbwa kwa Kiswahili.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Yemi alimuweka wazi mtu huyo kuwa ni kiongozi wa kundi la Sauti Sol linalobamba Afrika Mashariki aitwaye Bien Baraza.
“Asante kwa kupoteza muda wako na kutafsiri wimbo wangu wa No Gode kutoka Kiingereza na kuuweka kwa Kiswahili. Nakupenda sana!”Inasemekana Yemi Alade na Baraza wamekuwa karibu kuliko zamani hivyo huenda ni wapenzi kwani kwa mara ya kwanza walikutana nchini Kenya kwenye msimu huu wa Coke Studio, ambapo jumla ya wasanii 28 kutoka Uganda, Kenya, Tanzania, Msumbiji na Nigeria walikutana kwa ajili ya kufanya kazi pamoja za Coke.

0 comments :

Post a Comment