Home » » Picha: Rais Magufuli Avaa Sare za Jeshi Akiwa Arusha

Picha: Rais Magufuli Avaa Sare za Jeshi Akiwa Arusha

Written By Bewith Jeddy on Friday, January 22, 2016 | 4:28 PM

Magufuli Gwanda (6) Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wananchi wa Arusha Mjini wakati akipita Barabarani kuelekea Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA) Monduli ambako pamoja na mambo mengine kesho Januari 23, anatarajiwa kutunuku Kamisheni kwa Maafisa wanafunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli kundi la 57/15.

Rais Magufuli akiwa amevalia sare za kijeshi amesimamishwa na kuwasalimu wananchi katika maeneo ya Sanawali, Tekniko, Ngarenalo, Mbauda, Majengo na Kisongo.

 
 
 Wananchi waliojitokeza kumlaki rais Magufuli.Rais Dkt Magufuli akiwasikiliza wananchi kwa makini alipopita maeneno ya Sanawali kuwasalimia wakati akielekea Wilayani Monduli.

0 comments :

Post a Comment