Home » » Msanii wa filamu apewa kichapo na mumewe

Msanii wa filamu apewa kichapo na mumewe

Written By Bewith Jeddy on Tuesday, January 19, 2016 | 8:45 AMAkiwa amejilaza baada ya kusababishiwa maumivu yaliyotokana na kipigo kutoka kwa mumewe.

WIVU wa mapenzi! Msanii maarufu wa filamu Bongo mkoani hapa, Sada Mohamed, yu hoi kitandani baada ya kupewa kichapo na mumewe, Said Maulid ’Zungu’ aliyechukizwa na kitendo cha mkewe huyo ‘kuekti’ filamu akimlilia kimahaba mwanaume mwingine, inayokwenda kwa jina la Think Before.

Tukio hilo la kushangaza ambalo kwa sasa ndiyo gumzo katika Mitaa ya Mji Kasoro Bahari kufuatia umaarufu wa Sada anayerusha sinema zake kupitia Runinga ya Abood, lilijiri juzikati nyumbani kwa wanandoa hao, Mtaa wa Mafisa Kata ya Mwembesongo mjini hapa kisha sakata hilo kutinga polisi na kufunguliwa jalada la kesi namba MOR/ RB.1485/2015- SHAMBULI, KUDHURU ambapo Zungu alikamatwa na kulala ndani kwa siku mbili kabla ya kuachiwa kwa dhamana.

Mwandishi wetu alimtafuta Zungu na alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo alisema: “Kweli nilimpiga mke wangu kwa kunidhalilisha ilihali akijua ni mke wa mtu.” Kwa sasa Zungu anasubiri kufikishwa mahakamani kujibu shitaka linalomkabili.

Source: GPL

0 comments :

Post a Comment