Home » » Mrembo yamkuta mazito India, afa

Mrembo yamkuta mazito India, afa

Written By Bewith Jeddy on Monday, January 25, 2016 | 3:19 PM

 Mariamu Salum akiwa hospitali.


DAR ES SALAAM: Inauma sana! Mrembo wa Kibongo, Mariamu Salum (29) yamemkuta mazito akiwa nchini India baada ya kuugua na kufariki dunia kufuatia kutelekezwa katika Uwanja wa Ndege wa New Delhi nchini humo.
Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichopo nchini humo, Mariamu alikwenda India Novemba, 2015 kwa rafiki yake aliyetajwa kwa jina moja la Nyamizi ambaye anadaiwa kuwapeleka warembo wa Kibongo nchini humo kwa ajili ya kujiuza.Akiwa katika pozi enzi za uhai wake.

“Nyamizi hushirikiana na mama mmoja, mkazi wa Magomeni (Dar) ambaye ni wakala wa kuwauza mabinti nje ya nchi kwa kuwadanganya kuna kazi za saluni lakini wakifika huko hunyang’anywa pasipoti na kulazimishwa kujiuza.
“Ujue India kumekuwa na biashara kubwa ya madanguro ya mabinti kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo Tanzania, Mariamu alivyokwenda India, viza yake ilikuwa ya miezi mitatu na ilionekana anakwenda kama mtalii lakini alifikishiwa kwenye moja ya madanguro hayo.
“Mariamu, akiwa huko alianza kuumwa, baada ya kuzidiwa na mwili wake kudhoofika, wenzake walianza kumcheka, kumkejeli, kumnyanyapaa na kumnyanyasa kwa kumpiga picha za kawaida na video kisha kuzituma kwenye makundi ya WhatsApp (Wikienda lina moja ya video hizo).
“Akiwa hoi kwa kuumwa, wenzake hao walimchukua na kumpeleka uwanja wa ndege kisha wakamtelekeza ambapo wasamaria wema walimpeleka katika Hospitali ya An Aple, India na hapo ndipo alipofariki dunia baada ya mateso makali na kutengwa,” kiliweka nukta chanzo.
Baada ya taarifa hizo Ijumaa Wikienda lilizungumza na baba wa marehemu, Salumu Ali ambaye alikiri mwanaye kutelekezwa nchini humo.
Naye kaka wa marehemu, Abdallah Kingwande ameishukuru serikali kwa kuhakikisha mwili wa Mariamu unarudishwa nchini lakini akaiomba serikali kuchunguza kifo cha ndugu yao.
Mwili wa marehemu Mariamu uliwasili nchini Alhamisi (wiki iliyopita) majira ya saa 9:30 alasiri na kuzikwa Ijumaa katika Makaburi ya Kimanzichana mkoani Pwani, ameacha watoto wawili.
APUMZIKE KWA AMANI!

Source: GPL

0 comments :

Post a Comment