Home » » Hatariii: bibi aiba viti mahakamni, kigogo wa mashtaka awajibika kumlipia dhamana

Hatariii: bibi aiba viti mahakamni, kigogo wa mashtaka awajibika kumlipia dhamana

Written By Bewith Jeddy on Friday, January 8, 2016 | 12:00 PMBibi mmoja mwenye umri wa miaka 87 mkazi wa nchini Kenya, anakabiliwa na kesi ya kuiba viti viwili vya plastic katika moja ya mahakama mjini Nairobi.

Bibi huyo aitwae Risper Ongwena, alizua gumzo kwenye mitandao ya kijamii juzi baada ya kituo cha televisheni Citizen kuripoti kuwa amerejeshwa rumande kwa kukosa dhamana.

Baada ya wakenya wengi kulizungumzia sana kwa ghadhabu, hatimae mkulugenzi wa makosa ya jinai na mwanasiasa maarufu nchini humo Mike Sonko leo wamejitokeza kumtoa rumande kwa dhamana bibi huyo.

Sonko na DPP walilazimika kuziacha mezani 5000ksh, na kuahidi kumrejesha mahakamani ifikapo Januari 19 mwaka huu.

0 comments :

Post a Comment