Home » » Fedheha! Mke Adaiwa Kuiba Fedha za Vicoba

Fedheha! Mke Adaiwa Kuiba Fedha za Vicoba

Written By Bewith Jeddy on Friday, January 22, 2016 | 11:26 AMMtuhumiwa, Mariam
Deogratius Mongela na Chande Abdallah, Ijumaa
Dar es Salaam: FADHILA ya Punda Mateke! Hakuna neno zuri linaloweza kutumika zaidi ya fedheha kwa mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Mariam anayedaiwa kuvunja droo na kuiba fedha taslimu shilingi laki tano, mali ya familia iliyompa hifadhi yeye na mumewe ambaye ni mgonjwa, Ijumaa linakupa zaidi.
Tukio hilo lilitokea Januari 10, mwaka huu huko Kigogo Fresh nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na baadaye ikagundulika kuwa fedha zilizoibwa, zilikuwa zimekopwa katika kikundi cha Vicoba na mwenyeji wao aliyetambuliwa kwa jina moja la Fatuma. Mke huyo alitoroka na kumtelekeza mumewe bila kujali nini kingemtokea.
“Yaani hata sielewi niseme nini, kama kulia nimelia sana kama unavyojua Vicoba hawaelewi suala la kuibiwa au pesa hujafanyia biashara, wanachotaka ni marejesho tu, kinachoniuma zaidi ni ubinadamu tuliomuonesha Mariam, kweli pesa yenyewe nimeipata tarehe 5 mwezi jana, na yeye anaiba mie nitarudisha vipi pesa ya Vicoba jamani?” alisema kwa malalamiko mwenyeji huyo.

Kwa mujibu wa mashuhuda, siku ya tukio Mariam alionekana kutotulia, mara kwa mara akidai kumkumbuka mama yake na kwamba endapo angepata nauli, wakati wowote angeondoka kwenda kumjulia hali.
Jitihada za kumtafuta Mariam ziligonga mwamba kwani simu yake ya mkononi haikupatikana kila ilipopigwa na hivyo kuwalazimu wafadhili hao kwenda Kituo cha Polisi Pugu na kumchukulia RB yenye namba PUG/RB/926/2016.

0 comments :

Post a Comment