Home » » Rais Magufuli atengua uteuzi wa Dk. Hosea

Rais Magufuli atengua uteuzi wa Dk. Hosea

Written By Bewith Jeddy on Thursday, December 17, 2015 | 10:30 AMDk. Edward Hosea

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.John Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa, Dk. Edward Hosea kuanzia leo kwa sababu yakutoridhishwa na utendaji wa taasisi hiyo.

Katika hatua nyingine Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, amesema, Rais John Pombe Magufuli ameagiza kusimamishwa kazi mara moja kwa watumishi wanne wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ambao walisafiri nje ya nchi licha ya Rais Magufuli kupiga marufuku safari za nje kwa Watumishi wa Umma.

Watumishi hao ni Mary Mosha, Ekwabi Mujungu, Doreen Kapwani na Rukia Nakitasi ambao walisafiri nje ya nchi licha ya kunyimwa kibali cha safari kutoka kwa Rais ama Katibu mkuu.
Balozi Sefue amewataka watumishi wengine wa umma kutii agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Magufuli na kuonya kuwa atakae kiuka atachukuliwa hatua Kali.

Source: GPL

0 comments :

Post a Comment