Home » » Rais Magufuli atangaza Baraza lake la Mawaziri

Rais Magufuli atangaza Baraza lake la Mawaziri

Written By Bewith Jeddy on Friday, December 11, 2015 | 9:45 AM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akitangaza baraza lake la mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 10, 2015.
Kulia kwake ni Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na kushoto ni Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akitangaza baraza lake la mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 10, 2015. Kulia kwake ni Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na kushoto ni Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa. Kushoto kabisa ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli hivi punde ametangaza baraza lake la mawaziri, amesema wizara nyingi wameunganisha na atakuwa na wizara 18, na watakuwa na mawaziri 19 tu, na baadhi ya wizara zitakuwa na manaibu waziri huku zingine hazitakuwa na manaibu waziri.
Magufuli: Kumekuwa na speculation nyingi na watanzania wamekuwa na hamu kubwa ya kujua baraza la mawaziri, baada ya kusubira kwa muda mrefu, baada ya kuapa tulitakiwa angalau tarehe kumi tuwe tumetangaza baraza.
Tuliona angalau tujiridhishe kwanza, baraza lililopita lilikuwa na mawaziri na manaibu zaidi ya 59, tukaona tuwe na baraza dogo. Hatuwezi kukaa bila baraza, katika baraza hili, wizara nyingi tumeziunganisha na kutakuwa na wizara 18 na tutakuwa na mawaziri 19 tu, kuna baadhi ya wizara zitakuwa na mawaziri na hazitakuwa na manaibu waziri.
Lengo ni kutimiza ahadi yetu ya kuwa na baraza dogo kupunguza gharama na effective kwa kufanya kazi. Zilitengwa bilioni 2, mawaziri watakapoteuliwa waende semina elezi, baraza nitakaloliteua halitakuwa na semina elekezi na fedha tutaelekeza sehemu nyingine kama ni madawati au kwenye elimu bure. Watafanya semina elekezi wenyewe ndani kwa ndani.
BARAZA LA MAWAZIRI
Wizara ya Ofisi ya Rais,Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora
Mawaziri – George Simbachawene  na Angela Kairuki
Naibu Waziri – Sumeilam Said Jaffo
Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Raisi, Muungano na Mazingira
Waziri – January Makamba
Naibu Waziri – Luhaga Joelson Mpina
Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi Vijana, Ajira na Walemavu
Waziri – Jenista Muhagama
MaNaibu – Dkt. Possy Abdallah na Anthony Mavunde
Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
Waziri – Mwigulu Nchemba
Naibu Waziri – William Ole Nasha
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Waziri Bado hajapatikana
Naibu Waziri – Inj. Edwin Ambandusi Ngonyani
Wizara ya Fedha na Mipango
Waziri Bado hajapatikana
Naibu Waziri – Ashantu Kizachi
Wizara ya Nishati na Madini
Waziri – Prof. Mwijarubi Muhongo
Naibu Waziri – Medard Kalemani
Wizara ya Katiba na Sheria,
Waziri – Harrison Mwakyembe
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afika Mashariki, Kikanda na Kimataifa
Waziri – Dk. Augustino Mahiga
Naibu Waziri – Dkt. Susan Kolimba.
Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
Waziri – Dk. Hussein Mwinyi
Wizara ya Mambo ya Ndani
Waziri – Charles Kitwanga.
Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Waziri – William Lukuvi
Naibu Waziri – Angelina Mabula
Wizara ya Maliasili na Utalii
Waziri Bado hajapatikana
Naibu Waziri– Inj. Ramol Makani
Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.
Waziri Charles Mwijage
Wizara ya Elimu,Sayansi Teknolojia na Ufundi
Waziri Bado hajapatikana
Naibu Waziri – Inj. Stella Manyanya
Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Waziri – Ummy Mwalim
Naibu Waziri –  Dkt. Hamis Kigwangalla
Wizara ya Habari, Utamadu, Wasanii na Michezo
Waziri – Nape Nnauye
Naibu Waziri – Anastasia Wambura
Wizara ya Maji na Umwagiliaji
Waziri – Prof. Makame Mbarawa
Naibu  Waziri– Inj. Isack Kamwela

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, makamu wa Rais, Waziri Mkuu na katibu mkuu kiongozi wakiwasili moja ya kumbi za mikutano ya ikulu kwa ajili ya Rais kutangaza Baraza la Mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam Desemba 10,2015.
 
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana kwa furaha na wanahabari mara baada ya kutangaza baraza lake la mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam Desemba 10, 2015.

Picha ya pamoja na Waandishi wa habari baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati akitangaza Baraza la Mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam Desemba10,2015

 
 
 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akirejea ofisini baada ya kutangaza baraza lake la mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 10, 2015. Kulia kwake ni Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na kushoto ni Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa. Kushoto kabisa ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue.
Swali: Kuna baadhi hukutaja, tatizo ni nini hasa kwa wizara ambazo hujateua? Wabunge wa chama chako hawana sifa? Usimamizi wa baraza unatarajia zitafanya kazi zake Dodoma ukiondoa TAMISEMI?
Magufuli: Nilitegemea ungeniuliza kwanini sikuteua siko niliyoteuliwa, subira yavuta heri, hawa wameanza na wengine watafata. Usiwe na haraka. Kuhusu Dodoma tutatekeleza yaliyoko kwenye ilani ya chama cha mapinduzi.
Swali: Umesema hakutakuwa na semina elekezi, utafanya nini waweze kwenda na kasi ya hapa kazi?
Magufuli: Niliyowachagua wote wana CCM na wengi wao ni wabunge, walinadi ya sera hapa kazi na ndio maana haja ya semina elekezi, spidi ni hiyo hiyo ndio maana hatutatumia semina elekezi ya bilioni mbili.
Manyerere Jackton: Kwa kupunguza ukubwa wa baraza la mawaziri na kwa kulinganisha na tulipotoka, serikali itakuwa imepunguza kiasi gani?
Magufuli: Wewe ndie utapiga hesabu, kwa vile ni mmiliki wa gazeti huwa unapiga hesabu huwa unapata kiasi gani. Utanisaidia katika kupunguza baraza tutakuwa tumesevu kiasi gani na zile tulizosevu za gharama elekezi, kuchelewa kutangaza baraza na wale ambao sijawataja na bahati nzuri nyie waandishi mnaweza kupiga hesabu vizuri. Zipo nchi zina mawaziri wengi mpaka kufikia hata 70, wizara 44, manaibu na mawaziri. Tutakapomaliza tutakuwa na baraza la watu 34 tu.
Wakienda kule mawaziri wakafanye kazi kweli ndio maana sisi tulipochaguliwa tulifanya kazie kweli na hatukwenda kwenye semina elekezi na tulijielekeza, wakajieleze kwenye maeneo yao.
Wasihangaike kufanya sherehe kwa sababu ni kazi ngumu na kama wapo wanaopenda kufanya sherehe wajiandae kufanya sherehe siku wakifukuzwa, contract ni miaka mitano. Wakawafanyie kazi watanzania bila kuwabagua, Baraza hili la wizara 15 tumejiridhisha linaweza kufanya kazi tunayowatarajia kuifanya effectivly. Ngoja tukimaliza uteuzi wote tutajua tumesave kiasi gani ili ziweze kwenda kwa wananchi.
Raymond(Uhai Production): Siku saba zimetimia, wafanyabiashara wamesharejesha zile hela?
Magufuli: Swali hilo kamuulize kamishna wa kodi TRA.
SWALI: Kuna wizara ina mawaziri wawili, huko kazi ngumu?
Magufuli: Kafanye utafiti hio wizara imeunganisha wizara ngapi, utapata majibu.
Swali: Katika baraza, kuna mawaziri wa baraza lililopita, ulizangatia nini wakati wa uteuzi?
Magufuli: Umekosea hata kupiga hesabu, Kafanye hesabu vizuri, waliorudi ni saba na sio kumi? Ukipiga utaelewa ni vigezo gani nilivyotumia.
Asanteni sana na ninawashukuru

0 comments :

Post a Comment