Home » » Pacha wa Wema ni gumzo

Pacha wa Wema ni gumzo

Written By Bewith Jeddy on Friday, December 4, 2015 | 1:34 PM

 Staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu akiwa na pacha wake.

Ule msemo kwamba duniani ni wawiliwawili umeonekana kuwa na nguvu baada ya kuwepo kwa binti mrembo anayefanana sana na staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu.


Binti huyo anayefahamika kwa jina la Tuerney ambaye pia ana shepu bomba, amekuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii hasa Instagram na Facebook kwani wadau wamekuwa wakiweka picha zake na za Wema kisha kuonesha jinsi walivyofanana.
Ijumaa lilifanya jitihada za kutaka kumjua kwa undani lakini katika kuonesha si mtu wa kutaka umaarufu kivile, alipotafutwa alikataa kutoa ushirikiano akisema yeye hataki mambo ya magazeti. Jionee picha!

0 comments :

Post a Comment