Home » » Mr. Nice ageukia ufugaji wa kuku

Mr. Nice ageukia ufugaji wa kuku

Written By Bewith Jeddy on Monday, December 14, 2015 | 11:51 AM



Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Mr Nice amepost picha akiwa kwenye banda la kuku na kuandika:
Sio mpaka niimbe tu ndio nipate hela. Hii pia ni moja kati ya kazi zinazonipa jeuri, some time nakaa kimya kabisa ila sharehe zinaendelea na wengine wanahisi ninabiashara haramu. Napenda kuwamshauri wasanii wenzangu mkishatoka kwenye majukwaa kile mnalichokipata wekezeni kidogo ili msiwe watumwa na vipaji vyenu kwamba lazima uimbe ndio hupate pesa.

Sisi wasanii wa Tanzania tunaweza kijimiliki lakini wengi wanapenda kumilikiwa ndo maana unakuta mtu kuanzia gari, nyumba hadi godoro unalolalia kumbe sio mali yake. Nashukuru kwenye mkumbo huo sijawahi ingia na nadhani wapo wasanii wachache pia ambao hawajawahi ingia hasa hawa wa Hip Hop walio wengi nawafahamu hitikadi zao kumilikiwa ni mwiko, ila wa bongofleva na bongomovie wengi wanapenda kitonga ndio maana hawafanikiwi. Kwa kasi ya JP Magufuli mnatakiwa mbadilike, kauli ya Hapa Kazi Tu itawanyoosha. Huu ni moja ya waraka wangu wa kishujaa na hauna chenga hata moja ni moja ya ujumbe wangu kwa mashabiki wangu.
Kuonesha kuwa hajafulia, hivi karibuni hitmaker huyo wa ‘Fagilia’ alionesha mjengo wake uliopo Chanika jijini Dar es Salaam.

0 comments :

Post a Comment