Home » » Mbunge nchini Kuwait afariki wakati wa kikao cha bunge

Mbunge nchini Kuwait afariki wakati wa kikao cha bunge

Written By Bewith Jeddy on Wednesday, December 23, 2015 | 9:30 AM

 Nabil al-Fadl enzi za uhai wake

MBUNGE wa Kuwait Nabil al-Fadl (65) amefariki dunia ghafla leo baada ya kuanguka kutoka kwenye kiti chake bungeni wakati wa kikao cha bunge la nchi hiyo.Bunge la Kuwait

Wabunge walimzingira na kutaharuki hali iliyojitokeza bungeni humo wakati Waziri wa Afya wan chi hiyo, Dkt Ali al-Obaidi akijaribu kumtibu hadi wakati madaktari walipowasili.
Marehemu Al-Fadl — ambaye alikuwa ni mwandishi wa habari alikuwa maarufu kwa kutumia jarida lake kuwaasa wabunge wenzake na hata wakati mwingine kuwakosoa.
Aidha Al-Fadl alifahamika zaidi kwa kuwakaripia waasi wa Kiislamu ambao aliwashambulia kwa maneno makali.
Wakati mmoja aliwashangaza wasomaji wake alipoitaka serikali iondoe mara moja marufuku ya uuzaji wa pombe na maeneo ya burudani.

CREDIT: Al Arabiya News Channel

0 comments :

Post a Comment