Home » » Maneja atumbuliwa jipu gesti

Maneja atumbuliwa jipu gesti

Written By Bewith Jeddy on Friday, December 18, 2015 | 9:05 AM

Akiwa haamini kilichotokea baada ya fumanizi hilo


SASA kinachoonekana ni tumbuatumbua majipu iliyoanzishwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli ‘JPM’ dhidi ya mafisadi imeenea kila kona ya nchi, mtu akiumbuliwa katika uovu wowote, wanasema ametumbiliwa jipu na ndivyo ilivyomtokea Salim ambaye ni meneja wa usimamizi wa mafuta kwenye ‘sheli’ zilizopo mkoani Pwani.

Hussein amejitambulisha kwa kikosi cha Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ cha Global Publishers kuwa yeye ni mume wa Farida. Kwa hiyo Farida ni mke wake hivyo kumlalamikia Salim kuwa, alimnasa na mkewe gesti.
Hussein anadai usiku wa Desemba 15, mwaka huu alimnasa Salim akiwa na mkewe huyo tena wa ndoa kwenye gesti moja iliyopo Misugusugu, Kibaha Mkoa wa Pwani.

WENDE PAMOJA NAYE Akisimulia kisa chake kwa OFM ndani ya gesti hiyo majira ya saa 9 usiku, Hussein alisema yeye na Farida wanaishi Mbezi Mwisho, Dar es Salaam.


amejaliwa kupata mtoto mmoja ambaye kwa sasa ananyonya.Anasema: “Nilishtukia mawasiliano mabaya kati ya Salim na mke wangu. Meseji za kumchombeza mke wangu ili wakutane. Huyu jamaa namfahamu, ananifahamu, naweza kusema ni rafiki yangu.
wa hiyo mke wangu ni kama shemeji yake. Ikaniuma sana kwani najua anaelewa mimi ni mume wa Farida.” MKE ASHINIKIZWA “Nilimuuliza mke wangu kwa nini ana mawasiliano hayo na Salim, akaniongopea kwamba eti meseji zilikosea namba na kuingia kwake.
“Nilimwambia kama ni kweli na ili turidhishane, wapange kukutana naye mahali kisha mimi niwashtukize kuwatokea ili aone kama Salim atajitetea sawasawa na utetezi wa mke wangu au la! Lengo kama ni kweli nimtumbue jipu kama mafisadi wanavyotumbuliwa na Magufuli siku hizi.

 Akiomba kusamehewa kwa kitendo alichokifanya


” SIKU YA TUKIO Mume huyo aliendelea kuiambia OFM kuwa, siku hiyo ya tukio, mkewe na Salim walipanga kukutana saa 3 usiku kwenye baa moja iliyopo Kibaha. Baada ya kukutana wakaenda eneo linaloitwa Kibaha kwa Mathias kisha wakatoka hapo mpaka Mlandizi.
“Kote walikokuwa wanakwenda mimi na mke wangu tulikuwa tunawasiliana. Mpaka inafika saa saba usiku, wao walikuwa bado kwenye mabaa wakipata vinywaji. Nyumbani kuna mtoto ananyonya,” alisema mume huyo.
Akaendelea: “Kufika saa nane, mke wangu akasema sasa wanakuja eneo linaitwa Misugusugu ambako kuna gesti. Nilichofanya, nilimpigia simu askari mmoja kutoka Kituo cha Polisi Visiga, akaja Misugusugu.

 Akijistili


“Alipofika, mke wangu na Salim wao walishazama chumbani muda. Ndipo tukawavamia na varangati likaibuka. Si unajua tena, mke anauma bwana. Na nyinyi mmetokea, sijui mmetoka wapi!”
OFM WALIFIKAJE? Ilikuwa saa saba na nusu usiku, mtu mmoja alimpigia simu kamanda wa OFM na kumtonya kuhusu kuwepo kwa varangati kwenye gesti hiyo lakini hakujua ilihusu nini. Wakati simu hiyo ikipigwa, OFM walikuwa maeneo ya Mbezi ya Kibanda cha Mkaa kuchunguza tukio moja la mfanyabiashara kudaiwa kuficha kontena eneo hilo.
Kwa kutumia pikipiki iendayo kasi, OFM waliweza kufika eneo hilo ndani ya dakika 22 kwa vile ilikuwa usiku hivyo hakukuwa na foleni kama mchana. Nje ya gesti hiyo, OFM walikuta wananchi wenye hasira wakiwa na mishale, walioamini kuwa, varangati ndani ya gesti hiyo, huenda kulikuwa na majambazi.Akiwa na pingu mkononi

Polisi aliyekutwa eneo la tukio anaitwa Romuhadi, alisema yeye aliitwa eneo hilo akiamini kuna uhalifu. Lakini kwa sababu alimkuta Hussein akimtuhumu Salim kumkuta na mke wake ndani ya gesti, ilibidi ampige pingu asikimbie ili kuimarisha usalama wa mtuhumiwa kwa vile nje kulikuwa na watu wengi, wakiwemo wahuni.
OFM KURUDI DAR,MTUHUMIWA, MTUHUMU KUELEKEA KITUONI Saa 9 na dakika kadhaa, Salim akiwa ndani ya pingu huku akiomba msamaha mara kwa mara kwa Hussein, OFM ilishika njia kurejea Dar na afande huyo ambaye ni Mkuu wa Kituo cha Polisi Visiga akiondoka na watu hao kuelekea kituoni kwa ajili ya dawati la jinsia ambalo hushughulika na matatizo kama hayo.

CHANZO: GPL

0 comments :

Post a Comment