Home » » Magufuli kuombewa Uingereza

Magufuli kuombewa Uingereza

Written By Bewith Jeddy on Wednesday, December 23, 2015 | 1:00 PMRais John Pombe Magufuli.

Na Gabriel Ng’osha

KASI ya Rais John Pombe Magufuli ‘JPM’ inazidi kuwashangaza wengi ambapo wachungaji wa Kanisa la Calvary Charismatic Baptist Church Swahili Service la jijini London, Uingereza wameamua kumfanyia maombi maalumu Jumatatu ijayo.
Maombi hayo yamepangwa kufanyika katika kanisa hilo lililopo 119 East India, Dock Road Poplar London EI46DE, huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Naibu Balozi wa Tanzania nchini humo, Msafiri Marwa na yataongozwa na kiongozi mkuu wa kanisa hilo, Bob Baraka, Loise Gitahi na Askofu Francis Sarpong sambamba na wahamasishaji Joe Matonda na Teddy Mpangala ambao wamewaomba Waafrika wajitokeze kwa wingi siku hiyo.
Akizungumza na gazeti hili, mmoja wa wahamasishaji wa tamasha hilo ambaye ni mfanyabiashara wa Kitanzania nchini humo, Chris Lukosi alisema kasi ya utendaji wa kiongozi huyo wa Tanzania imewavutia Waafrika wengi wanaoishi Uingereza.
“Rais amekuwa gumzo kila kona, Waafrika na wasomi wanaoishi nje wanamkubali na kutamani kuona Bara la Afrika likipata viongozi kama yeye,” alisema.

0 comments :

Post a Comment