Home » » Jux afunguka haya juu ya mjengo wake na harakati za masomo nchini China,soma hapa livee

Jux afunguka haya juu ya mjengo wake na harakati za masomo nchini China,soma hapa livee

Written By Bewith Jeddy on Tuesday, December 15, 2015 | 3:02 PMMsanii Jux ambaye kwa sasa anatamba na kazi yake mpya 'One more night' amefunguka na kuweka wazi kuhusu mjengo wake wa ghorofa ambao miezi kadhaa aliuonesha kwenye mitandoa ya kijamii.

 Jux alidai kuwa kwa sasa amesimama kidogo kuendeleza mjengo na kuwekeza pesa katika kufanya muziki ikiwa pamoja na kuendelea kufanya video zenye ubora.

"Unajua kwa sasa kidogo nimesimama kuendeleza nyumba hivyo ipo siku watu watakuja kuona mjengo ukiwa umekamilika maana maisha yetu sisi wasanii hayawezi kufichika, nimesimama sababu pesa nazopata nimezielekeza katika kufanya muziki na video kali" Alisema Jux.

Katika hatua nyingine tulitaka kufahamu anawezaje kufanya video kali ambazo zinamgharimu pesa nyingi na mwisho wa siku haonekani akifanya show nyingi kama wasanii wengine au mara nyingine baada ya kutoa video hizo anaondoka kabisa nchini na kwenda china, katika hili Jux alikuwa na haya ya kusema.

Ni kweli hata Jumatatu (Jana) nitaondoka na kurudi shule nchini china lakini kwa sasa nachofanya ni kuwekeza katika muziki huku nikiamini baadaye hiki nachofanya sasa kitanilipa, hivyo najenga ukaribu na mashabiki zangu na Mungu akijalia nikamaliza masomo yangu nchini China nitaanza kufanya show za uhakika, unakuta hata sasa hivi natafutwa sana ili nifanye show lakini bahati mbaya huwa nakuwa nje ya nchi na kuzikosa show hizo" Aliongezea Jux

Msanii Jux anasema amewaomba mashabiki zake wamvumilie amalize shule na kupata shahada yake ya kwanza ndipo atakuwa huru zaidi na kazi ya muziki kwani sasa shule bado inambana ndiyo maana anashindwa kufanya show nyingi na anaonekana kwa msimu msimu.

STORY NA EATV

0 comments :

Post a Comment