Home » » Fundi anaswa na denti wa secondary chumbani

Fundi anaswa na denti wa secondary chumbani

Written By Bewith Jeddy on Saturday, December 12, 2015 | 11:19 AM

 Sadiq akiwa haamini baada ya kufumaniwa na mwanafunzi


Kibano! Licha ya Rais John Pombe Magufuli kuchimba mkwara na kutangaza kuhakikisha watoto wa Kitanzania wanapatiwa elimu ya uhakika, tena bure kuanzia shule ya msingi hadi kidato cha nne, kijana aliyefahamika kwa jina la Sadiq, mkazi wa Mbande-Kisiwani, Mbagala jijini Dar anashikiliwa na polisi akituhumiwa kunaswa chumbani na denti wa sekondari akivunja amri ya sita.

 Mwanafunzi huyo akilia baada ya fumanizi


Sadiq ambaye ni fundi wa kuchomea mageti alikamatwa juzikati akiwa kitandani kwenye chumba chake katika nyumba moja iliyopo maeneo hayo ya Mbande-Kisiwani akiwa na mwanafunzi huyo (jina kapuni) wa kidato cha pili katika shule moja maarufu ya wasichana jijini Dar.
TAARIFA KUTOKA KWA MSAMARIA MWEMA
Chanzo cha tukio hilo ni taarifa ya msamaria mwema aliyepiga simu ofisi za gazeti hili kwenye Kitengo cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) akieleza jinsi ambavyo binti huyo anayetokea kusikojulikana akiwa na sare za shule amekuwa akiingia chumbani kwa Sadiq kisha kufanya mambo yao kwa zaidi ya saa 10 kwa siku.

BINTI AENDA KUOGA NA KANGA MOJA NYEPESI

Mtoa habari wetu huyo alieleza kwamba, wawili hao wakishajifungia ndani kwa muda mrefu, binti huyo huonekana akitoka kwenda bafuni kuoga huku akiwa na kanga moja.

OFM HAWALAZI DAMU
Ilielezwa kwamba, kitendo hicho kilionekana kuwakera majirani hao ambao waliona dawa pekee ya kukomesha uovu huo ni kuwajulisha OFM ambao huwa hawalazi damu katika eneo hilo hasa kwa kitendo hicho kinacholenga kuwaumiza wazazi wanaosomesha mabinti zao.

Baada ya kupewa taarifa hizo, OFM ilimfungia kazi kijana huyo anayetuhumiwa kuharibu ‘mtoto wa shule’ ambapo iliwapanga makachero wake.
Ili kuwahi eneo la tukio, makachero hao walitumia pikipiki iendayo kwa kasi kuelekea eneo husika ambapo walifika kwenye nyumba hiyo na kujiridhisha kuwa wawili hao bado walikuwa chumbani.

 Nguo za mwanafunzi huyo baada ya fumanizi


RIPOTI POLISI
Hata hivyo, kama kawaida yake, OFM ilikwenda kuripoti polisi katika Kituo cha Mbande ambapo baada ya kumweleza mkuu wa kituo hicho kisa kamili, walipewa ushirikiano mkubwa wa kumtia mbaroni mtuhumiwa huyo.

OFM ilipewa afande mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Koplo Lipingu aliyeungana na mjumbe wa eneo hilo, Uwesu Kisoma kwa ajili ya kuongeza nguvu kuonesha kuwa ni tukio lisilokubalika katika jamii.
BINTI KAMA ALIVYOZALIWA
Timu nzima ilipofika kwenye nyumba hiyo ilikuwa tuliii, kama vile hakuna watu lakini mjumbe alipobisha hodi ndipo mlango ukafunguliwa na fundi huyo aliyekuwa tayari kavaa nguo.

Msafara huo ulipoingia chumbani ulikutana uso kwa uso na binti huyo akiwa kitandani huku begi lake la madaftari na vikorokoro vingine vikiwa sakafuni.


BINTI AANGUA KILIO
Baada ya kunaswa live na OFM kujitambulisha, binti huyo alianza kuangua kilio kwa uchungu akiomba msamaha kwani baba yake ni mkali na anaweza kumdhuru akisikia taarifa hizo.

HAPA KAZI TU
Kutokana na utendaji wa serikali mpya wa ‘Hapa Kazi Tu’, OFM nao wameimarisha kikosi chao na kukataa rushwa wala aina yoyote ya kuiminya habari hiyo na kuwaongoza afande na mjumbe kurudi kituoni kwa ajili ya kufungua kesi.Akiwa na begi lake
 
MAMA AANGUA KILIO
Msafara huo, ukiwa njiani, OFM walimuomba denti huyo namba za wazazi wake ambapo walimpigia baba yake lakini alisema alikuwa njiani akitokea Mtwara kisha wakampigia mama yake mlezi aliyejitambulisha kwa jina la Mwanaid ambaye baada ya kufika kituoni hapo aliangua kilio.

KESI MBAGALA-KIZUIANI
Kutokana na uzito wa kesi hiyo, Kituo Kidogo cha Polisi cha Mbande waliihamishia katika Kituo cha Polisi cha Mbagala-Kizuiani kwa ajili ya kufungua mashtaka.

0 comments :

Post a Comment