Home » » Bomoa bomoa yawafikia wananchi wanaoishi pembezoni mwa bonde la mto Msimbazi jijini Dar es Salaam

Bomoa bomoa yawafikia wananchi wanaoishi pembezoni mwa bonde la mto Msimbazi jijini Dar es Salaam

Written By Bewith Jeddy on Thursday, December 17, 2015 | 4:14 PM

Mkuu wa Kitengo cha Sheria Balaza la Taifa la usimamizi wa mazingira Tanzania (NEMC), Manchale Heche akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam juu ya zoezi la Bomoabomoa maeneo ya miundombinu na maeneo yote hatarishi nakuwataka wananchi waliojenga katika fukwe za bahari Kingo za mito na mikondo ya bahari kuhamisha mali zao mapema.

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na Manispaa za jiji la Dar es salaam zitafanya zoezi la kuondoa wavamizi maeneo yote ya Mabondeni, kingo za mito na za Bahari, maeneo ya wazi, maeneo ya miundombinu na maeneo yote hatarishi zaidi ya 150 katika jiji la Dar es salaam. Bomoa bomoa ya leo inaendelea katika Bonde la mto msimbazi.

Wananchi wakitoa samani pamoja na vitu mbalimbali ndani ya nyumba zao ili kupisha ubomoaji wa nyumba zilizo maeneo hatarishi.

 
 
 

0 comments :

Post a Comment