Home » » Balozi Sefue: maagizo ya Rais Magufuli hayavunji sheria ya ununuzi

Balozi Sefue: maagizo ya Rais Magufuli hayavunji sheria ya ununuzi

Written By Bewith Jeddy on Monday, December 7, 2015 | 1:00 PMKatibu mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema maagizo ya Rais  Magufuli kutaka fedha zilizokuwa zitumike kwa matumizi yasiyo ya lazima, kupelekwa katika miradi mbalimbali ya maendeleo nchini, hayavunji sheria ya manunuzi wala utaratibu mwingine wa kisheria.
Aligiza pia Bilioni 4 zilizokuwa zitumike katika sherehe za Uhuru Disemba 9 zitumike kupanua barabara ya Mwenge- Morocco.
Akitoa ufafanuzi wa barabara ya Mwenge-Morocco, Balozi Sefue  amesema mradi huo sio mpya na kwamba taratibu zote zilishafuatwa ikiwa ni pamoja na kuwalipa waliokuwa wamejenga  kando ya barabara.

Amesema kilichokuwa kinakwamisha mradi huo ni  pesa.
Akizungumzia sakata la wakuu wa mikoa na wilaya kuwanyima likizo wafanyakazi huku wengine  wakitiwa rumande kwa masaa  6, Balozi Sefue  amesema serikali haina taarifa rasmi hivyo akalitaka shirikisho la vyama vya wafanyakazi (Tucta) kuwasilisha malalamiko serikalini badala ya kuishia kulalamika katika vyombo vya habari.

0 comments :

Post a Comment