Home » » Uturuki yaitungua ndege ya Urusi

Uturuki yaitungua ndege ya Urusi

Written By Bewith Jeddy on Tuesday, November 24, 2015 | 2:52 PM

JESHI la Uturuki kwa kutumia ndege zake za kivita F-16, limeitungua na kuilipua ndege ya kivita ya Urusi aina ya Sukhoi Su-24, karibu na mpaka wake na nchi ya Syria leo asubuhi, Ankara na Moscow zimethibitisha kutokea kwa shambulizi hilo.


Maofisa wa Usalama nchini Uturuki wamesema kuwa, Jeshi lao limeamua kuchukua hatua hiyo baada ya agizo lao la mara kwa mara kuitaka Urusi isipitishe ndege zake za kivita kwenye anga la Uturuki karibu na mpaka wa Syria, japo Urusi wamekaidi agizo hilo.

Kwa upande wake, Jeshi la Ulinzi nchini Urusi wajitetea kuwa ndege yao haikuwa kwenye anga la Uturuki bali ilikuwa kwenye anga la Syria wakati Waturuki wakiishambulia.

Vyombo vya habari vya Utruruki vimesema kuwa, vimenasa picha zikionesha marubani wawili wakiruka kwa parachute na kuokoka wakati ndege hiyo ikiteketea angani kabla ya kutua.

0 comments :

Post a Comment