Home » » Shehe: Magufuli aongezewe ulinzi

Shehe: Magufuli aongezewe ulinzi

Written By Bewith Jeddy on Tuesday, November 24, 2015 | 11:00 AM
Katibu Mkuu wa Mashehe na Wanazuoni nchini, Shehe Hamisi Mataka


 
KUTOKANA na hotuba kali na yenye matumaini aliyoitoa Rais John Magufuli mwishoni mwa wiki wakati anafungua Bunge la 11, baadhi ya viongozi wa dini wameshauri kiongozi huyo wa nchi aongezewe ulinzi.
Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti, viongozi hao walisema Magufuli ni mchapakazi na kauli yake ya kupambana na mafisadi ni nzuri lakini inapaswa iende sambamba na ulinzi wa kutosha.
Katibu Mkuu wa Mashehe na Wanazuoni nchini, Shehe Hamisi Mataka alipohojiwa na gazeti hili alisema:
“Rais Magufuli ni tunu ya taifa, Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa ni mchapakazi, inafaa walindwe kuliko kawaida kwa sababu kazi wanayoifanya ni ya taifa kwa faida ya taifa.
“Wote hawa nawafahamu ni wachapakazi na wana nguvu ya kutumikia taifa kwani wote hufuatilia kazi na siyo watu wa kukaa ofisini.”
Alisema anamuombea Rais Magufuli na waziri mkuu wake afya njema ili waweze kutumikia taifa kama walivyoahidi na ana imani kuwa Watanzania watagundua baada ya siku si nyingi kwamba hawakufanya makosa kumchagua kuongoza nchi.
Akimzungumzia Waziri Mkuu, Majaliwa, Shehe huyo alisema ni mtu anayeweza kuendana na kasi ya Magufuli.

0 comments :

Post a Comment