Home » » Mtangazaji Prince Baina Kamkuru afariki dunia

Mtangazaji Prince Baina Kamkuru afariki dunia

Written By Bewith Jeddy on Friday, November 20, 2015 | 5:00 PMPrince Baina Kamkuru enzi za uhai wake

Mtangazaji wa zamani wa Radio Free Afria (RFA), Clouds FM na Star TV, Prince Baina Kamkuru amefariki dunia ghafla jana usiku akiwa jijini Dar es Salaam.
Taarifa za awali kuhusu kifo cha marehemu Kamkuru zinaeleza kuwa alianguka ghafla wakati akifanya mazoezi ya viungo na alipokuwa akiwahishwa hospitali kwa matibabu alifariki dunia.
Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa kwenda mkoani Kagera kwa mazishi siku ya Jumapili na kwa sasa msiba upo Kigamboni jijini Dar.

0 comments :

Post a Comment