Home » » Majibu ya rufaa ya Sepp Blatter na Michel Platini ni haya

Majibu ya rufaa ya Sepp Blatter na Michel Platini ni haya

Written By Bewith Jeddy on Thursday, November 19, 2015 | 10:36 AMMichel Platini wa kulia na Sepp Blatter


November 18 headlines za Rais wa shirikisho la soka ulimwenguni (FIFA) Sepp Blatter na Rais wa shirikisho la soka barani Ulaya UEFA Michel Platini wamerudi tena katika headlines baada ya kufungiwa katika soka kwa siku 90. Blatter na Platini walifungiwa siku 90 kwa makosa kadhaa ikiwemo na matumizi mabovu ya fedha.
Kufuatia maamuzi ya kufungiwa kwa viongozi hao kwa siku 90 ili uchunguzi ufanyike kwa makosa yao, kabla ya wawili hao kuamua kukata rufaa, Blatter na Platini ambao walikata rufaa kupinga kufungiwa huko, November 18 ndio rufaa yao imetolewa majibu na kukataliwa na FIFA.


Kwa pamoja Blatter na Platini walifungiwa na waendesha mashitaka wa Uswiss October 7 wakitajwa kufanya makosa kadhaa ikiwemo ya utawala mbovu, kosa la Blatter kumlipa Platini dola milioni 2 kinyume na taratibu, fedha ambazo zinatajwa kuwa zilitumika kufanya kampeni za Blatter kuendelea kuwa madarakani.
Hata hivyo kutupiliwa mbali kwa rufaa hiyo kunazidi kumkatisha tamaa Michel Platini kugombea Urais wa FIFA utakaofanyika utaofanyika February 26 2016 Zurich ambapo Blatter atakuwa anaachia nafasi ya Urais wa FIFA rasmi toka aitumikie kwa miaka 17 na kutangaza kujiuzulu baada ya tuhuma hizo.

0 comments :

Post a Comment