Home » » Balozi Sefue akagua Muhimbili

Balozi Sefue akagua Muhimbili

Written By Bewith Jeddy on Tuesday, November 24, 2015 | 9:59 AM

Balozi Ombeni Sefue alipowasili katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili akisalimiana na wafanyakazi wa hospitali hiyo.
 Balozi Sefue (kushoto) akiendelea kusalimia wafanyakazi wa hospitalini hapo mara baada ya kushuka kwenye gari lake.
 Mashine ya MRI ikiwa katika chumba maalum
Mashine ya CT-SCAN iliyopo kwenye matengenezo ambapo Balozi Sefue ameelezwa itatengemaa ndani ya muda wa siku mbili.
Kushoto kwake Balozi Sefue ni Fundi wa kutengeneza CT-SCAN ambaye ni mwakilishi kutoka Kampuni ya Philips akitoa ufafanuzi kwa balozi huyo ambao ndiyo wauzaji wa mashine hizo, Kevin Omollo Biomedical Engineer.

Fundi Kevin Omollo akiwa mbele ya CT-SCAN inayodaiwa kuwa katika matengenezo huku akitoa maelekezo kwa Balozi Sefue sambamba na baadhi ya viongozi kutoka Wizara ya Afya.

 Mgonjwa akifurahia kuondokana na adha ya kulala chini baada ya kupata vitanda.

Balozi Sefue akimjulia hali mgonjwa aliyekuwa amelazwa kwenye moja ya vitanda vilivyonunuliwa

 Akiendelea kuona wagonjwa.

 Wagonjwa wakiwa wamelazwa kwenye vitanda vilivyonulunuliwa.
 Mmoja wa watangazaji wa EATV, Noah Laltaika akiangalia ubora wa vitanda hivyo.Mwonekana wa vitanda hivyo
Balozi Sefue akitoa ufafanuzi wa jambo mara baada ya kukagua mashine za CT-Scan, MRI na vitanda.

KATIBU Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue leo ametembelea katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kukagua Mashine za MRI CT-Scan ikiwa ni ziara ya mrejesho wa pili wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli wakati alipotembelea hospitalini hapo na kukuta mashine hizo zikiwa mbovu.
Balozi Sefue amezikuta mashine hizo zikiwa bado kwenye matengenezo ambapo mafundi kutoka nchini Kenya ambao ndiyo wasambazaji wa bidhaa za Philips walikuwa wakitengeneza, hivyo wakaahidi kuwa baada ya siku mbili mashine ya MRI itakuwa imetengemaa na CT-Scan kufikia siku ya Alhamisi itakuwa nayo imetengemaa.
Balozi Sefue mara baada ya kupata maelekezo hayo amewatahadharisha kutoendelea kupata tena usumbufu wa mashine hizo na kusema hatua kali zitachukuliwa endapo watafanya mzaha dhidi ya mashine hizo.
Baada ya ukaguzi wa mashine hizo, Balozi Sefue alitembelea kwenye jengo jipya la kitengo cha Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (Moi) kuangalia vitanda vilivyonunuliwa kutokana na agizo la Rais Magufuli kuamuru pesa zilizokuwa zimeandaliwa kwa ajili ya bajeti ya sherehe za ufunguzi wa Bunge 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dodoma alhamisi iliyopita kupelekwa kununulia vitanda Muhimbili. 

Source: GPL 

0 comments :

Post a Comment