Home » » Bastola ya Ray yazua hofu ukumbini!

Bastola ya Ray yazua hofu ukumbini!

Written By Bewith Jeddy on Thursday, August 6, 2015 | 11:21 AMStaa wa filamu Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ 

Bastola inayomilikiwa na staa wa filamu Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ imezua hofu na taharuki kubwa miongoni mwa watu walioiona hadharani, Amani lilikuwepo.
Sekeseke hilo lilijiri hivi karibuni ndani ya Ukumbi wa Regency uliopo Mikocheni jijini Dar kulikokuwa na sherehe ya kuzaliwa (bethidei) ya mnenguaji wa Kundi la Wasafi Classic Baby (WCB) la mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Moses Iyobo ambaye pia ni mzazi mwenzake mwigizaji Aunt Ezekiel Grayson.
Awali, mwandishi wetu alimshuhudia Ray akiwa ‘amechangamka’ huku akizungumza na kila
mtu na vicheko vya kumwaga.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, ilianza kusikika minong’ono baada ya Ray kunyanyua mkono wa kulia, jambo lililomfanya mwanahabari wetu kutaka kujua zaidi.
Baada ya ‘kung’arisha’ macho zaidi ndipo alibaini ‘mguu wa kuku’ (bastola) ya msanii huyo ikiwa nje na kuamua kumpiga picha nyingi za ushahidi.
“Mmh! Kwa nini asiwe mwangalifu wa kutunza bastola yake? Sasa ndiyo nini? Ona bastola iko nje nje, mwenzetu anatutia hofu,” alisikika msanii mmoja jina tunalihifadhi aliyekuwa karibu na mwandishi wetu.
Jitihada za kzungumza na Ray juu ya ishu hiyo, ziligonga mwamba baada ya msanii huyo kudai hakuwa na muda wa mazungumzo kwa wakati huo.

0 comments :

Post a Comment