Home » » Nape azungumzia sababu za kuchelewa kwa Vikao vya CCM

Nape azungumzia sababu za kuchelewa kwa Vikao vya CCM

Written By Bewith Jeddy on Friday, July 10, 2015 | 11:19 AM


Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari nje ya Ukumbi wa White House, Mjini Dodoma leo Julai 10, 2015.

KATIBU wa NEC, Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi, Nape Nnauye amesema, leo hii majina matano ya makada wa chama hicho walioomba kuteuliwa na CCM kuwania kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, yatajulikana, na kufuatia majina matatu ya makada hao ambayo yatapelekwa mbele ya Mkutano Mkuu utakaofanyika Jumamosi Julai 11, 2015.


Nape amesema vikao vyote vinaanza leo saa nne, na hakuna kikao chochote kilichokwisha fanyika ikiwa ni pamoja na kile kinachozungumzwa sana na vyombo vya habari yaani kikao cha kamati ya maadili ya chama hicho ambacho ndicho kinachokata majina na kutoa mapendekezo Kamati Kuu.
Alipoulizwa ucheleweshwaji huo umetokana na nini, Nape alisema "Nyote mmeshuhudia, Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, amekuwa na kazi nyingi katika kipindi cha siku mbili hizi na hivyo asingeweza kusimamia vikao hivyo kama ilivyotarajiwa ingawa amedokeza kuwa "wakubwa" hao walikuwa wakikutana kwa majadiliano na wadau ingawa hakueleza ni wadau
gani.

0 comments :

Post a Comment