Home » » Mke ampa kipigo wifi yake

Mke ampa kipigo wifi yake

Written By Bewith Jeddy on Monday, July 20, 2015 | 12:54 PMEster Mjila anayedaiwa kumjeruhi wifi yake.Idd ya nuksi! Wakati watu wakijiandaa kwa mnuso wa Sikukuu ya Idd wikiendi iliyopita, mambo yameenda kombo katika familia ya mwanamke aliyetajwa kwa jina la Ester Mjila anayedaiwa kuwapa kipigo mama mkwe na wifi yake, Mage Sibonike akiwatuhumu kumtafutia mchepuko
mumewe.

Katika tukio hilo la kutisha lilijiri hivi karibuni maeneo ya Soweto mkoani Mbeya ilidaiwa kwamba, Ester alikuwa akimshuku mumewe kuwa ana mchepuko. Chanzo chetu kilidai kwamba, katika maisha yao, Ester na mumewe wamejaliwa mtoto mmoja.
Ilisemekana kwamba, siku ya tukio, Ester alimfuatilia mumewe ambapo aligundua kuwa anakwenda kuonana na mwanamke aliyetajwa kwa jina Fetty Mchina, karibu na nyumbani kwa mama mkwe wake.


 Mage Sibonike akiwa na maumivu makali baada ya kupewa kichapo na wifi yake.


Ilidaiwa kuwa, baada ya Ester kutega kwa muda mrefu maeneo hayo, alimuona mzazi mwenziye huyo akiwa kwenye grosari ya dada yake aliyetajwa kwa jina moja la Mage, wakiwa kimalavidavi na Fetty Mchina huku pembeni yao akiwemo wifi yake huyo.
Ilielezwa kwamba, uvumilivu ulimshinda ndipo akaanzisha timbwili ‘hevi’ bila kuuliza ambapo katika varangati hilo huku chupa zikirushwa, mumewe na Fetty Mchina walitoka nduki na kumuachia msala wifi mtu.
Ilidadavuliwa kwamba, katika hali ya kushangaza umati uliofurika na kufunga mtaa, baada ya kutandikana makonde, Ester alivunja chupa tupu ya bia ambayo aliitumia kumchanachana wifi yake huyo na kumsababishia majeraha makubwa mwilini.

 Moja ya jeraha mguuni.


Chanzo hicho kiliendelea kutiririka kuwa, mama mkwe aliyekuwa nje nyumbani kwake alisikia mayowe na kufika eneo la tukio ndipo Ester akamuhamishia kipigo mama mkwe wake kwa kumzaba makofi hadi akapoteza fahamu.
Ilielezwa kwamba, baada ya Ester kuondoka eneo hilo, mumewe alifika na kumchukua dada yake aliyekuwa hajiwezi na kumpeleka Hospitali ya Rufaa ya Mbeya baada ya kupata PF-3 kisha Ester alikamatwa na kuwekwa ndani katika Kituo cha Kati Mbeya Mjini kabla ya kuachiwa kwa dhamana.

 Akizungumza kwa majonzi, mama mkwe huyo alisema kuwa alishangaa baada ya kusikia mwanaye akipiga kelele na alipotoka aliona akipigwa na kuchanwa na chupa na wifi yake.

 Jeraha alilolipata usoni.

Alisema alipoingilia kati alipokea kipigo kutoka kwa Ester hadi akapoteza fahamu.
“Nilimkuta mwanangu anakwanguliwa kwa chupa, nilipojaribu kuamulia ndipo nikapewa kipigo na mkwe wangu hadi nikazimia,” alisema mama huyo aliyegoma kutaja jina lake.Kaka mtu.

Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Mage ambaye bado anauguza majeraha alisema kuwa alishtukia akivamiwa na mke wa kaka yake na kuchanwa kwa chupa akituhumiwa kumuunganishia wanawake kaka yake, jambo ambalo siyo kweli

0 comments :

Post a Comment