Home » » Mhe. Magufuli apokelewa kwa kishindo Dar, ahutubia nyomi Mbagala

Mhe. Magufuli apokelewa kwa kishindo Dar, ahutubia nyomi Mbagala

Written By Bewith Jeddy on Wednesday, July 15, 2015 | 10:00 AM


 Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na mgombea mwenza Mhe. Samia Suluhu Hassan wakiteremka kwenye ndege.

 Makada na wanachama wa CCM wakijiandaa kuwapokea viongozi hao.

Wanachama wa chama hicho waliojitokeza kumsikiliza kwenye Uwanja wa Zakheem, Mbagala jijini Dar.Waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda hawakuwa nyuma katika shamrashamra hizo

MGOMBEA wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dk. John Pombe Joseph Magufuli, leo ametambulishwa rasmi kwa wakazi wa Jiji la Dar, ambapo amepokelewa kwa kishindo na makada wa chama hicho katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) na kuelekea Mbagala - Zakheem ambako alizungumza na wakazi wa jiji la Dar. 

0 comments :

Post a Comment