Home » » Mfanyakazi Clouds mbaroni

Mfanyakazi Clouds mbaroni

Written By Bewith Jeddy on Saturday, July 18, 2015 | 12:08 PM

MREMBO aliyetajwa kwa jina la Cynthia Maximillian ambaye alikuwa mfanyakazi wa Kampuni ya Clouds Media Group  amejikuta akitiwa mbaroni kwa madai ya kutapeli mamilioni ya shilingi ya wafanyakazi wenzake na marafiki aliosoma nao.

Taarifa zilizotua kwenye gazeti hili zinadai kuwa, Cynthia alitiwa rumande katika kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar Julai 13, mwaka huu.

Ilidaiwa kuwa, mrembo huyo ambaye kwa sasa ameachishwa kazi kwenye kampuni hiyo
aliwakusanya marafiki zake na kuwapa mchongo kuwa, kuna viwanja vinapatikana huko Bagamoyo kwa shilingi mil1.5 kupitia Chama cha Mazingira Fukayosi.
“Baada ya kuona fursa tulijikusanya na kumpa Cythia pesa, kila mmoja alitoa milioni moja na nusu, na tulikuwa watu kama mia hivi akiwemo bosi Ruge Mutahaba. Cha ajabu baada ya kukamata mshiko huo akaleta usanii,” alidai mmoja wa wafanyakazi waliolizwa aliyeomba hifadhi ya jina lake.

Kufuatia utapeli huo, Cynthia alisakwa na kufikishwa polisi kisha kufunguliwa jalada la kesi lenye namba; OB/IR/6025/2015 KUJIPATIA FEDHA KWA NJIA YA UDANGANYIFU.
Baada ya kuzipata taarifa hizo, mwandishi wetu aliongea na Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds, Ruge Mutahaba ambaye alikiri kuwa miongoni mwa waliolizwa wamo wafanyakazi wa Clouds akiwemo yeye.

“Ni kweli hata mimi Cynthia ameniingiza mjini na tumepata taarifa za kutiwa kwake mbaroni ila watu wajue kwamba kwa sasa siyo mfanyakazi wetu maana tayari alikuwa ameshaachishwa kazi. Wananchi wajue kwamba sisi kama Clouds hatuhusiki na utapeli huo bali ni waathirika,” alisema Ruge.

Source: GPL

0 comments :

Post a Comment