Home » » Mayweather apokonywa taji alilomshinda Pacquiao

Mayweather apokonywa taji alilomshinda Pacquiao

Written By Bewith Jeddy on Wednesday, July 8, 2015 | 3:47 PM

Bondia Bingwa wa dunia wa uzani wa Welter, Floyd Mayweather amepokonywa mkanda alioutwaa baada ya kumchapa Mfilipino Manny Pacquiao mwezi Mei mwaka huu.

Mmarekani huyo mwenye umri wa miaka 38 anadaiwa kushindwa kuilipa shirikisho la ndondi la
WBO ada ya dola laki mbili ($200,000), pesa alizotakiwa kulipa kabla ya Julai 3 mwaka huu.
Mayweather alitakiwa pia kutoa Mkanda wa Chipukizi wa WBO punde baada ya kumshinda Mfilipino Pacquiao kwa wingi wa alama.
Kufuatia kauli hiyo ya shirikisho la ndondi la WBO, Mayweather hatambuliwi tena kama anashikilia taji hilo badala yake taji hilo linashikiliwa na Mmarekani mwenza Timothy Bradley.
Yamkini Mayweather alikuwa ameiahidi WBO kuwa akimshinda Pacquiao, angevua mataji yote ya vijana ili kuwapa mabondia wapya fursa ya kuwania mataji hayo lakini hadi kufikia sasa hajafanya hivyo.
Taarifa yao iliyochapishwa katika mtandao wa wboboxing.com imesema kuwa, ''hatukukuwa na lingine baada ya Mayweather kushindwa kutekeleza matakwa yetu. kwa hivyo hatutamtambua Mayweather kama anashikilia Mkanda huo wa Welter'' Mayweather, ambaye ndiye anayeshikilia mataji ya WBA na WBC ana hadi Julai 20 kukata rufaa ya kauli hiyo.
Mayweather anatarajiwa kuandaa pigano lingine Mjini Las Vegas, Septemba 12, japo haijabainika atazichapa dhidi ya nani.
Wakati hayo yakijiri WBO inapanga pigano la Welter linalopangwa kufanyika kati ya Bradley na Jessie Vargas hivi karibuni.

NA BBC0 comments :

Post a Comment