Home » » Magufuli ndiye mgombea Urais wa CCM 2015

Magufuli ndiye mgombea Urais wa CCM 2015

Written By Bewith Jeddy on Monday, July 13, 2015 | 9:41 AMMBUNGE wa Biharamulo Mashariki (CCM) na Waziri wa Ujenzi, Mhe. John Pombe Magufuli ameshinda katika uchaguzi wa kumpata mgombea urais wa CCM kwa mwaka 2015. Magufuli ameshinda baada ya kupata jumla ya kura 2104 sawa na 87.1%, Balozi Amina Salum Ali amepata kura 253 sawa na 10.5% na Dk. Asha-Rose Migiro 59 sawa na 2.4%.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Anne Makinda ndiye aliyepewa jukumu la kutangaza mshindi aliyepatikana kwa kura za Kikao cha Mkutano Mkuu wa CCM kilichofanyika kuanzia jana na kuendelea leo asubuhi mkoani Dodoma.
KURA ZILIZOPIGWA: 2422
KURA ZILIZOHARIBIKA: 6
KURA HALALI: 2416

0 comments :

Post a Comment