Home » » Mshukiwa wa mauaji ya watu tisa kanisani nchini Marekani akamatwa

Mshukiwa wa mauaji ya watu tisa kanisani nchini Marekani akamatwa

Written By Bewith Jeddy on Saturday, June 20, 2015 | 8:42 PM

  Dylann Storm Roof baada ya kukamatwa na polisi.

  Roof akiwa chini ya ulinzi.
  Dylann Storm Roof akiwa ametiwa pingu.
  Roof akiwa na gari aina ya Hyundai alilokimbia nalo baada ya kutekeleza shambulio
 

Waumini wa Kanisa la Methodist wakifanya maombi, siku ya shambulio.

 
Carolina Kaskazini, Marekani
JESHI la ulinzi la Marekani limemkamata mshukiwa wa mauaji ya watu tisa katika Kanisa la Methodist la kihistoria mjini Carolina Kusini, Dylann Storm Roof, na kumpeleka gerezani kusubiri kufunguliwa mashtaka yanayomkabiri.
Vyombo vya usalama vya Marekani vinasema, Bw. Roof mwenye umri wa miaka 21 alikamatwa huko Selby Carolina Kaskazini umbali wa maili 250 kutoka eneo ambapo shambulizi hilo lilitekelezwa (Kanisa la Methodist) saa 13 baada ya shambulizi kabla ya kupandishwa ndege na kupelekwa mahabusu.
Maofisa wa Polisi wanasema kuwa mshukiwa huyo aliyejihami kwa bunduki aliketi katika mkutano wa mafundisho ya biblia kwa takriban saa moja kabla ya kufyatua risasi na kuwaua wanawake sita na wanaume watatu akiwemo mchungaji wa kanisa hilo usiku Jumatano.
Maofisa wamelitaja shambulizi hilo kama la uhalifu wa chuki na ubaguzi wa rangi.
Aidha Mwanasheria Mkuu Bi. Lorreta Lynch, amesema Idara ya haki itaangazia maswala yote ili kubaini mwafaka ya kumfungulia mashtaka mshukiwa.
Roof alitekeleza shambulio hilo ndani ya kanisa la Emmanuel African Methodist Church maarufu kama AME, kanisa linaloaminika kuwa la zamani zaidi linalotumiwa na watu wa asili ya Afrika nchini Marekani na kuwaua watu tisa wakiwemo wanawake sita na wanaume watatu miongoni mwao akiwa ni mchungaji wa kanisa hilo, Clementa Pinckney.
CHANZO NA DAILY MAIL

0 comments :

Post a Comment