Home » » Akutwa akichimbia mayai kwa dada yake

Akutwa akichimbia mayai kwa dada yake

Written By Bewith Jeddy on Saturday, June 20, 2015 | 8:08 PM

 KATIKA hali ya kushangaza mwanamke mmoja, Pili  Danji Mlapakalo amedaiwa kukutwa akifukia mayai viza kwenye dirisha la dada yake Hanifa Danji Mlapakalo kwenye nyumba wanayoishi iliyopo Mtaa wa Kisogo, Kata ya Kiwanja cha Ndege mkoani hapa.
  Pili  Danji Mlapakalo anayedaiwa kufukia mayai viza.

Tukio hilo lilitokea Juni 15, mwaka huu saa 11 alfajiri na kusababisha vurugu kubwa kati ya Hanifa na mdogo wake Pili, jambo lililosababisha umati wa watu kufurika eneo la tukio
wakiwemo ndugu wengine wa familia hiyo.
Dada mkubwa wa ndugu hao, Saida Danji Mlapakolo ambaye ni mtoto wa kwanza katika familia hiyo baada ya kuona wadogo zake wamekamatana uchawi aliamua kwenda kuomba ushauri kwa baba yao mdogo aitwaye Rajabu Mlapakolo ambaye alimshauri kwenda serikali ya mtaa kwa kuwa yeye alikuwa mgonjwa.
“Ni kweli mdogo wangu Pili alifumwa na mpangaji wetu akifukia mayai viza na kitambaa cheusi kwenye dirisha la chumba cha marehemu baba ambacho kwa sasa anaishi Hanifa,” alisema Saida na kuongeza kuwa nyumba hiyo wanaishi wapangaji na wadogo zake hao wawili.

Akionyesha sehemu alipoyafukia.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Kisogo, Salum Shaban alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na alisema waliitisha kikao ambapo Pili alipoulizwa alikiri kuchimbia vitu hivyo.“Baada ya majadiliano nilimuamuru Pili akavitoe vitu hivyo na akatekeleza, hivyo sasa amani imerejea.
Naye Pili alipoulizwa kuhusu sakata hilo alisema: “Ni kweli niliweka vitu hivyo ikiwa ni kinga yangu na wanangu kwa sababu dada yangu naye alikuja na mganga wakazunguka nyumba bila kunishirikisha.”
Hata hivyo, kauli hiyo ilimchefua Hanifa ambaye alisema kama ni kinga yake kwa nini asiweka kwenye dirisha lake?
Katika hatua nyingine siku iliyofuta ndugu mwingine wa familia hiyo, Fatuma Danji Mlapakolo anayeishi Sultan Area alimsihi mwandishi wetu asitoe habari hiyo gazetini kwa madai kuwa baba yao alikuwa maarufu sana hapo mjini, hivyo ikitoka itakuwa aibu kwao.

Source: GPL

0 comments :

Post a Comment