Home » » Aunt Ezekiel ajifungua mtoto wa kike

Aunt Ezekiel ajifungua mtoto wa kike

Written By Bewith Jeddy on Friday, May 22, 2015 | 2:28 PMStaa wa filamu nchini, Aunt Ezekiel.

STAA wa filamu nchini, Aunt Ezekiel amebahatika kupata mtoto wa kike kwa kujifungua salama, jana mchana katika hospitali binafsi iliyopo Mbezi jijini Dar, baada ya kufanyiwa upasuaji.


Akizungumza huku akiwa mwenye furaha, Aunt alisema kuwa anamshukuru Mungu kwa kila jambo kwa kuwa yeye ndiye muweza na aliyefanikisha safari yake hiyo salama, hivyo anamshukuru kwani sasa na yeye anaitwa mama.“Jamani Mungu ni mwema sana safari ilikuwa na vikwazo vingi lakini namshukuru sana nimefanikiwa kupata rafiki yangu mzuri anayeitwa Cookie na ninajivunia kuwa mama, naamini nitakuwa mama bora,” alisema Aunt.
Baba wa mtoto huyo ambaye ni dansa wa mwanamuziki Nassib Abdul ‘Diamond’, Moses Iyobo naye alionekana kuwa na furaha ambapo alisema amefurahi kuona mpenzi wake amejifungua salama na anamshukuru Mungu kwa kufanikisha hilo.
“Asante sana Mungu, Mungu ndiyo kamfikisha mpenzi wangu salama katika safari yake, name sasa naitwa baba,” alisema Iyobo.


0 comments :

Post a Comment