Home » » Mtoto afanyiwa bethidei, afariki dunia

Mtoto afanyiwa bethidei, afariki dunia

Written By Bewith Jeddy on Monday, April 27, 2015 | 10:10 AMInauma sana! Mtoto mzuri wa kiume aitwaye Jumanne Mwinyimbegu, mwenye umri wa mwaka mmoja amefariki dunia ghafla muda mfupi baada ya kufanyiwa sherehe ya kutimiza mwaka mmoja ‘bethidei’.


Tukio hilo la kusikitisha lilijiri nyumbani kwa wazazi wa Jumanne Mtaa wa Saadan Kata ya Mwembesongo mkoani hapa mwishoni mwa wiki iliyopita na kuibua simanzi nzito kwa kuwa alikuwa haumwi na ilikuwa muda mfupi baada ya kukata keki, kulishwa na kuimbiwa ‘happy bethidei tuyuuuuu’.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda kwa uchungu mama mzazi wa mtoto huyo, Khadija Salum alisema: “Inaniuma sana jamani. Jumanne ni mtoto wangu pekee ambaye ametimiza umri wa
mwaka mmoja. Nikaona nimfanyie ‘bethidei’.
“Niliwashirikisha majirani zangu, cha ajabu baada ya sherehe kukamilika majira ya saa 3:00 usiku mwanangu alijisikia uchomvu, nikaenda kumlaza lakini hakuamka tena.
“Nimemkimbiza kwenye Zahanati ya Ngeta (Mwembesongo), nilipofika manesi walimcheki wakaniambia mbona amekufa muda mrefu, nikarudi nyumbani nikiwa nalia,” alisema Khadija na kuongeza:
“Baada ya uchunguzi wa madaktari ilibainika kuwa kilichomuua mwanangu ni upungufu wa damu mwilini lakini niliwaambia alikuwa haumwi na alifurahia bethidei vizuri na wenzake.”
Mwili wa mtoto huyo ulihifadhiwa kwenye Makaburi ya Kola huku wana familia wakimwachia Mungu kwani kuna waliotaka kuhusisha tukio hilo na ushirikina.

GPL

0 comments :

Post a Comment