Home » » Wafanyabiashara Mwanza wagoma, kisa mwenyekiti wao kunyimwa dhamana

Wafanyabiashara Mwanza wagoma, kisa mwenyekiti wao kunyimwa dhamana

Written By Bewith Jeddy on Saturday, March 28, 2015 | 10:00 AM


Baadhi ya maduka katika mitaa mbalimbali mkoani Mwanza yakiwa yamefungwa huku wananchi wakihangaika kutafuta huduma hiyo.
 
WAFANYABIASHARA wanaofanya shughuli zao kwenye Mtaa wa Liberty jijini Mwanza, wamegoma kufanya biashara zao wakidai mwenyekiti wa chama cha wafanya biashara hapa nchini aliyekamatwa Dodoma kwa kosa la kuwahamasisha wafanyabiashara wasilipe kodi, aachiwe kutokana na kuwa hana kosa lolote.
Wakizungumza na vyombo vya habari, wafanya biashara hao wanaofanya hao   wamesema:  “Sisi tumechoshwa na tabia ya serikali kumkamata mwenyekiti wetu kwa madai kuwa alituhamasisha kutolipa kodi, jambo ambalo si kweli hivyo na sisi tutaendelea na mgomo huu kuishinikiza serikali
kumuachia mwenyekiti wetu.”
Aidha, wafanyabiashara hao wameongeza kuwa imekuwa ni kawaida yao kutofanya biashara siku ambayo mwenyekiti wao huwa anakwenda kusikiliza kesi yake lakini kwa sababu serikali, kupitia mahakama,  imekataa kutoa mdhamana kwa mwenyekiti wao,hawafungui maduka mpaka hapo atakapoachiwa.
Mgomo huo wa wafanyabiashara ulianza tangu jana Alhamisi  ambapo wafanyabiashara wote wa mtaa huo waligoma kufungua maduka yao wakitaka serikali imwachie mwenyekiti wao aliyekamatwa mjini Dodoma kwa madai kuwa amewachochea wafanya biashara hao wasilipe kodi.
Nao wananchi wa jijini hapa wameeleza kero wanazokutana nazo wakati maduka hayo yanapokuwa yamefungwaambapo wanakosa mahitaji yao na hivyo kuathiri vibaya maisha yao.
Katika hatua nyingine,mtaahuo ambao mahitaji muhimu ya binadamu hupatikana, wafanyabiashara mbalimbali kutoka Ukerewe, Igombe, Sengerema na hata mkoani Geita ambao huja kuchukua mahitaji hapo, wamesema mgomo huo umeathiri vibaya hali katika maeneo yao.

0 comments :

Post a Comment