Home » » Muendesha pikipiki apigwa rirasi shingoni na kuporwa pikipiki mkoani Morogoro

Muendesha pikipiki apigwa rirasi shingoni na kuporwa pikipiki mkoani Morogoro

Written By Bewith Jeddy on Thursday, February 5, 2015 | 10:54 AMMtu mmoja mikocheni wilayani mvomero mkoani Morogoro ameuwawa kwa kupigwa risasi shingoni na kisha kuporwa pikipiki aina Boxer ambapo jeshi la polisi linawashikilia watu watatu waliohusika na tukio hilo.
Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Leonard Paulo amesema jeshi la polisi lilifika katika eneo la tukio nakufanikiwa kuwakamata watu watatu wanasadikiwa kujihusisha na tukio hilo na linaendelea kuwahoji kisha watafikishwa mahakamani.
Aidha kamanda Paulo amesema jeshi la polisi linaendelea kumtafuta mtuhumiwa aliye kimbia ambapo katika hatua nyingine wamefanikiwa kumkamata hawara wa mtu huyo aliyejulikana
kwa majina ya Husuna Isimaeli mkazi wa mkindo ambaye alikuwa akimhifadhi mtuhumiwa  na jeshi la polisi litaendelea kumshikilia kwa mahojiano ilikumpata mtuhumiwa aliye kimbia.

0 comments :

Post a Comment