Home » » Mama aruka kwenye baiskeli, agongwa, afa!

Mama aruka kwenye baiskeli, agongwa, afa!

Written By Bewith Jeddy on Monday, February 9, 2015 | 10:07 AM

 Kaka wa marehemu(Sarah Joseph ), Tabu Joseph Ihuya akisimulia mkasa huo.


Majonzi! Mama mmoja mkazi wa Kijiji cha Lubuga wilayani Misungwi mkoani hapa, Sarah Joseph (22), amegongwa na lori lenye namba za usajili T 115 AVE lililokuwa likitokea Mwanza kwenda Dar kisha kufa papohapo baada ya kuruka kutoka kwenye baiskeli.
Tukio lilitokea hivi karibuni wilayani humo ambapo Sarah alikuwa amepakizwa kwenye baiskeli na mumewe ndipo lori hilo lilipomgonga na kumsababishia umauti.
Kwa mujibu wa kaka wa marehemu aitwaye Tabu Joseph, Sarah alipatwa na umauti aliporuka
kutoka kwenye baiskeli aliyokuwa amebebwa na mumewe ili kulikwepa lori hilo.

 Waombolezaji wakimzika marehemu Sarah Joseph aliyefariki kwa ajali


“Alikuwa ameolewa Kijiji cha Mwamanga hapa Misungwi na mumewe, Shija Lucas.
“Siku ya tukio alianza safari na mumewe kwenda Lubuga, nyumbani kwao (mke).
“Wakiwa barabarani waliliona lori hilo likiwa limepoteza mwelekeo wakajaribu kulikwepa.
“Ilibidi Sarah aruke kwenye baiskeli akijaribu kujiokoa lakini baada ya kuruka tu lori likawa limemfikia na kumgonga kisha likatoka kabisa barabarani.

Kaburi la marehemu Sarah Joseph

“Lakini baadaye lile lori liliingia tena barabarani na kuendelea na safari,” alisema Tabu.
Alisema kuwa, kwa msaada wa wasamaria wema kutoa taarifa, polisi walilifuatilia lori hilo hadi walipolikamata katika Kijiji cha Mwanangwa, Misungwi ndipo wakalirudisha hadi Kituo cha Polisi cha Misungwi ambapo dereva wake alishikiliwa.
Marehemu Sarah ameacha mtoto mmoja wa kiume mwenye umri wa miaka mitatu.

0 comments :

Post a Comment