Home » » Askari polisi aliyeuawa kikatili aagwa mkoani Dodoma

Askari polisi aliyeuawa kikatili aagwa mkoani Dodoma

Written By Bewith Jeddy on Friday, February 6, 2015 | 2:16 PM

 Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Ernest Mangu akiongoza waombolezaji katika kutoa heshima za mwisho kwa Askari  Namba G. 7168 PC JOSEPH ISACK SWAI aliyeuwawa huko
Chang’ombe ya juu mkoani Dodoma na mtu aliyefahamika kwa jina la TISSI SIRIL MALYA.


 Maombolezo wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa askari huyo shujaa


Wasifu wa marehemu ukisomwa

Na Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma
KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME – SACP amesema kama alivyotoa taarifa juzi tarehe 04/02/2015 kuhusiana na kuawa kwa Askari  Namba G. 7168 PC JOSEPH ISACK SWAI huko Chang’ombe ya juu mkoani Dodoma na mtu aliyefahamika kwa jina la TISSI S/O SIRIL MALYA.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dododoma lilianza msako wa kumtafuta mtuhumiwa huyo baada ya kufanya kitendo hicho cha kinyama cha kumkata kata kwa panga kichwani na mikononi askari huyo.
Kamanda MISIME amesema majira ya saa 23:00hrs usiku wananchi walimuona maeneo ya Mti Mkavu Mailimbili mkoani Dodoma akiwa bado na lile panga alilotumia kumuua askari. 
Hata hivyo walichukua sheria mkononi na kumshambulia sehemu mbalimbali za mwili wake, Polisi walifika eneo la tukio na kumchukua kisha kumkimbiza Hospitali ya Mkoa lakini daktari akagundua ameshafariki.
Aidha Kamanda MISIME amesema mtuhumiwa huyo katika kumbukumbu tulizonazo ni kwamba mwaka 2006 aliwahi kufungwa miaka mitatu (3) kwa kosa la kujeruhi, Pia mwaka 2009 alifungwa tena miezi sita (6) kwa kosa la kutishia kuua.
Ametoa pongezi kwa wananchi kwa kuonyesha kuchukizwa na kitendo alichomtendea askari wetu lakini waache kujichukulia sheria mkononi.
Pia ametoa wito kwa wananchi waanze kuchukua hatua kurekebisha maadili kuanzia ngazi ya familia kwani imeelezwa kuwa mtuhumiwa alikuwa ni mvutaji bangi kiasi kwamba ilimfanya awe anafanya vitendo ambavyo ni kinyume na maadili na sheria za nchi.

0 comments :

Post a Comment