Home » » Zari alala kwa Mama Diamond

Zari alala kwa Mama Diamond

Written By Bewith Jeddy on Thursday, January 15, 2015 | 9:34 AMMrembo wa Uganda, Zarinah Hassan ‘Zari’

IMEFICHUKA! Mrembo wa Uganda ambaye kwa sasa ndiye ‘usingizi’ wa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Zarinah Hassan ‘Zari’ hivi karibuni alitua Bongo na kulala nyumbani kwa mama wa Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’, Sinza-Mori jijini Dar.
Chanzo makini kilicho karibu na familia ya Diamond kimepenyeza ‘ubuyu’ kuwa, Zari alipata
fursa ya kupiga ‘mbonji’ nyumbani hapo alipomtembelea Diamond.
“Alikuja akambonji kwa mama Diamond kama siku mbili hivi halafu wakaondoka wote wakati Diamond alipokwenda Nigeria kwenye shoo ya Mwanasoka Bora wa Afrika 2014.
“Awali, Diamond alitaka akamlaze hotelini lakini mtoto wa kike akakataa, akasema anataka kuangusha usingizi nyumbani kwa mkwewe, Diamond akasema ruksa mama,” kilisema chanzo hicho.
Kikizidi kumwaga data, chanzo kilisema, mbali na kulala, Zari alishiriki kazi za ndani ikiwemo kupika na kupakua kama ilivyokuwa kwa zilipendwa wa Diamond, Penniel Mungilwa ‘Penny’ na Wema Sepetu.
Alipoulizwa Diamond kuhusiana na suala hilo hakutaka kufafanua mengi zaidi ya kukiri kwamba mrembo huyo alikuja Dar na kuondoka naye.


“Wewe jua alikuja, nikaondoka naye hayo mambo mengine siwezi kuyazungumzia,” alisema Diamond.
Amani lilipomtafuta mama Diamond kwa njia ya simu hakupatikana lakini mtu wa karibu alisema kwa sasa hatumii simu kwa sababu ambazo hazikutajwa.

Source: GPL

0 comments :

Post a Comment