Home » » Vikongwe Wapigana Mabusu Hadharani....!!!

Vikongwe Wapigana Mabusu Hadharani....!!!

Written By Bewith Jeddy on Thursday, January 22, 2015 | 10:00 AMMohamed Khalfan ambaye ni kikongwe wa miaka 78 mwenye ulemavu wa ukoma na mkewe, Habiba Shomari (68) hivi karibuni waliwashangaza watu baada ya kuamua kumwagiana mabusu hadharani.
Tukio hilo lilijiri kwenye Kambi ya Walemavu wa Ukoma ya Chazi iliyopo Kata ya Chazi wilayani Mvomero mkoani Morogoro ambapo kulikuwa na kikao cha serikali za mtaa kutatua mgogoro wa ardhi. 
Akizungumza  huku akiwa na furaha, Mzee Khalfan alisema ndoa yake na mkewe ina miaka 60, walifunga mwaka 1955 mkoani hapa.
”Nampenda sana mpenzi wangu huyu. Nilifunga naye ndoa mwaka 55, ila kwa bahati Mungu
hakutujalia kupata mtoto hata mmoja.
  “Lakini pamoja na kukosa mtoto hata wa dawa, tunaishi na mwezangu katika mapenzi mazito. Kila siku namwona kama mchumba na yeye ananiona kama mvulana mbichi kabisa,” alisema kikongwe huyo mwenye meno ya kuhesabu na kuwafanya watu wawapongeze hasa ikizingatiwa kuwa, ndoa za siku hizi zikidumu miaka miwili Mungu mkubwa!
Muda mwingi vikongwe hao walikuwa wakipelekeana midomo na kumwaga mabusu mazito. Baadhi ya watu walisema kwa kizazi cha sasa kuna cha kujifunza kwa vikongwe hao ingawa wenyewe walidai siri ya ndoa yao kudumu ni kuvumiliana na kuheshimiana.
Credit: Gazeti la Amani.

0 comments :

Post a Comment