Home » » Msanii wa Marekani Suge Knight akamatwa kwa mauaji

Msanii wa Marekani Suge Knight akamatwa kwa mauaji

Written By Bewith Jeddy on Saturday, January 31, 2015 | 12:41 PMMsanii wa muziki wa rap kutoka Marekani Marion Suge Knight

Polisi nchini Los Angeles inasema kuwa msanii wa muziki wa rap kutoka Marekani Marion Suge Knight amekamatwa kutokana na mashtaka ya mauaji baada ya kumgonga mtu mmoja na gari
lake hadi kumuua na baadaye kutoroka.Polisi wanasema kuwa Knight alijibizana na watu wawili katika eneo la kuegesha magari na baadaye kumgonga mmoja wao huku mwengine akijeruhiwa vibaya.
Wakili wake anasema ilikuwa ajali na kudai kuwa mteja wake alishambuliwa na watu wawili.
Suge Knight ni mwanzilishi wa kampuni ya Death Row Records ambayo iliwazindua wasanii maarufu wa mziki wa rap akiwemo Snoop Dogg na marehemu Tupac Shakur.

0 comments :

Post a Comment