Home » » Mrembo: nimesali bila nguo freemason

Mrembo: nimesali bila nguo freemason

Written By Bewith Jeddy on Monday, January 26, 2015 | 11:10 AMMrembo, Happiness Wilfred Nassari (27) anayedai kushiriki imani ya kifreemason

 INATOSHA! Mrembo, Happiness Wilfred Nassari (27), ameibuka na kudai kuwa amekuwa akisali bila nguo kwenye ibada ya imani ya Freemason inayosifika kwa ushirikina.Katika mahojiano yaliyofanyika hivi karibuni ndani ya chumba cha habari, makao makuu ya gazeti hili Bamaga, Mwenge jijini Dar, Happiness alisema kuwa, alianza kuingia kwenye imani hiyo kwa kwa kupitia kaka yake mmoja (jina tunalo) ambaye ni tajiri wa kupindukia kutokana na kuwa
mshiriki wa Freemason.
“Nilipojiunga ilikuwa si kwa matakwa yangu, kwani nilianza kwa kupata matatizo ya kuumwa magonjwa ya ajabuajabu, ikiwemo kutokwa na wadudu usoni kiasi cha kunitoa vidonda,” alisema mrembo huyo huku akionesha makovu ya vidonda hivyo.

“Hali ilipokuwa mbaya, ilibidi niende kwa mganga mmoja wa kienyeji ambaye aliniambia nimetupiwa majini ya kunuka ambayo yanabadilika harufu kila mara, lakini alitaka nimlipe shilingi milioni 5 ili anitibie, nikashindwa, nikaondoka.
“Kuna wakati vile vidonda vilisababisha nianze kufuatwa na nzi wengi hadi watu wengine wakawa wanadai kusikia harufu, ndipo nikaenda kwenye Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), Arusha  kwa Mchungaji Olduvic kuombewa ndipo nzi wakatoweka na harufu kupungua,” alisema.

0 comments :

Post a Comment