Home » » Mamba wala watu wauawa Sengerema

Mamba wala watu wauawa Sengerema

Written By Bewith Jeddy on Thursday, January 22, 2015 | 10:15 AM

Mmojawapo Mwanakijiji akiweka pozi juu ya mzoga wa mamba kuonesha furaha yake

WANAKIJIJI  wa Kome-Mchangani wilayani Sengerema mkoani Mwanza, wamewaua mamba
wawili wanaodaiwa kuua watu wawili na kuwajeruhi watu watatu.Mzee aliyewatega mamba hao (aliyeketi) akiwa nyuma ya mzoga wa mamba

Mamba hao waliokuwa katika kingo za Ziwa Victoria kijijini hapo, walitajwa kuwa kero kubwa kiasi cha kusababisha baadhi ya shughuli za kuinua uchumi katika kijiji hicho kama vile uvuvi na umwagiliaji kusimama kwa muda huku wanakijiji wakiwa na hofu ya kuliwa na mamba hao.

Wakizungumza na paparazi, wanakijiji hao walidai kuwa mara kadhaa walifikisha malalamiko yao kwa viongozi wa serikali lakini hakuna hatua zilizochukuliwa,  jambo lililowafanya wachange pesa na kumpa mzee mmoja ambaye alitumia mbinu za kitaalamu kuwatega mamba hao na hatimaye kuwaua.

0 comments :

Post a Comment