Home » » Madereva wa daladala wagoma kutoa huduma jijini Arusha leo

Madereva wa daladala wagoma kutoa huduma jijini Arusha leo

Written By Bewith Jeddy on Wednesday, January 21, 2015 | 2:58 PMBaadhi ya wanafunzi wakiwa kwenye lori kutokana na mgomo wa daladala. Picha na Maktaba Yetu)

MADEREVA Daladala jijini Arusha,leo wamefanya mgomo wa kutoa huduma ya kusafirisha abiria katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo kwa kile kinachodaiwa kugomea kuanzishwa kwa safari mpya wanayotakiwa kuianza hivi sasa.

Wakazi wa maeneo mengi ya jiji hilo wanalazimika kutembea kwa miguu, huku wengine wenye uwezo kidogo wakitumia usafiri wa bodaboda ili kuwahi katika shughuli zao za kuendelea
kujitafutia chochote. Askari Polisi na Wanamgambo wamesambaa kila kona jijini Arusha.

Safari zenye mgogoro zaidi ni zile za Kutoka Njiro na Moshono kuelekea mjini.

Source: GPL

0 comments :

Post a Comment