Home » » Maajabu ya kobe kwenye chimbo la papaso!

Maajabu ya kobe kwenye chimbo la papaso!

Written By Bewith Jeddy on Monday, January 26, 2015 | 10:31 AMKobe ni mnyama jamii ya Reptilia ambaye kwa kumtazama tu lazima ujiulize maswali mengi.Kitendo chake cha kuficha kichwa, mwendo wake na gamba lake gumu!!
Kobe huyuhuyu unayemfahamu Team papaso inakuletea mambo kumi na moja unayotakiwa kuyajua kuhusiana na kobe!!!
#KOBE hawezi kuogelea kabisa lakini anaweza kubana pumzi zake kwa muda mrefu sana!! Ukimwondoa Nng’e kobe anafuata kwa uwezo wa kuishi muda mrefu bila kupumua!!!
#KOBE wamekuwa ulimwenguni zaidi ya miaka milioni mia mbili iliyopita!!! Ni zaidi ya mijusi
na wanyama wengine!!
#KOBE wa sasa unaowafahamu wanaweza kuishi hadi miaka mia moja!!
#KOBE wameweza kuishi kila bara kasoro bara moja tu Antarctica!!
#Gamba la kobe limeundwa na mifupa 60 tofauti tofauti!! Na mifupa hii yote imeungana.
#Kobe wa kike hutaga kati ya mayai mawili hadi kumi na mawili na huchukua siku 90 hadi 120

kuyaatamia na hatimae kutotoa.
#Kobe wa kike ana uwezo wa kutaga kila baada ya miaka mitatu baada ya kukutana na kobe dume!!
#Kobe hana meno mpenzi msikilizaji!!
#Licha ya kuwa na gamba gumu sana, kobe akiguswa hata na unyoya wa kuku anatambua kuwa ameguswa!! Ana hisia kali sana!!
#Kobe mkubwa kabisa duniani ana uzito wa kilogram mia saba.. hii inamfanya kuwa reptilia mzito kupita wote!!
#Kuna aina 40 ya kobe!!!

Huyu ndiye kobe………
Tukutane tena katika chimbo la papaso siku ya jumatatu.. ili ujifunze, na kuburudika Zaidi!!!
Haya yote ni katika PAPASO Pekee!!!

0 comments :

Post a Comment