Home » » Kasisi wa kwanza mwanamke kuapishwa nchini Uingereza leo

Kasisi wa kwanza mwanamke kuapishwa nchini Uingereza leo

Written By Bewith Jeddy on Monday, January 26, 2015 | 2:45 PMLibby Lane

KANISA la Stockport la nchini Uingereza leo litamwapisha mwanamke wa kwanza kuwa kasisi.
Libby Lane mwenye umri wa miaka 48 na ambaye ana watoto wawili atakuwa kasisi wa kwanza wa kanisa hilo la Anglikana.

Sherehe hizo zitaongozwa na kasisi Mkuu, John Sentamu eneo la York Minister.
Hatua hiyo inayomaliza ukiritimba wa utamaduni wa wanaume kuwa makasisi umeendelea
kuzua hisia tofauti miongoni mwa wafuasi wa kanisa hilo la Kianglikana duniani.

0 comments :

Post a Comment