Home » » Ishu ya Wema Sepetu kuhusu kumdai Diamond, majibu ya Wema ni haya hapa

Ishu ya Wema Sepetu kuhusu kumdai Diamond, majibu ya Wema ni haya hapa

Written By Bewith Jeddy on Friday, January 23, 2015 | 1:00 PMUkubwa wa story hii ambayo jana aliizungumzia Martin Kadinda, Meneja wa Wema Sepetu imefanya millardayo.com kumtafuta Wema ili kuujua undani zaidi juu ya ishu hii ambayo ilichukua headlines kuandikwa Magazetini na mitandaoni pia.
Kwenye Exclusive Interview, Wema Sepetu amesema haya;
Taarifa hii imenishtua sana maana asubuhi ya jana nimekuta kwenye gazeti wameandika nikashangaa yaani hapa nimekaa kwa sababu muda mwingi siendeshi mimi akaunti yangu ya twitter, anaiendesha mtu wangu wa blog Bestizo maana nilikua nataka kutoa tamko-- Wema Sepetu.
Nilishasema ukurasa huu tulishaufunga na nilishasema haiwezi kujirudia tena, nashangaa watu wanarudi na maneno yale yale maana nimekaa kimya kwa kila kitu ili kuepuka haya maneno
Hakuna kitu ambacho namdai Diamond,hakuna siku hata moja nimefikiria kwenda kumshtaki
Diamond labda kama kungekuwa kuna kitu chochote, yaani labda kungekuwa na ukweli wa kitu chochote siwezi kupoteza muda wangu kwenda polisi, sijawahi kufanya kitu cha namna hii hizi taarifa zimenishtua sana
Sijawahi kujiunga VICOBA maana sivijui, nilikua nimekaa na mtu akanambia labda Wema hujui  hawa watu wa VICOBA wanajaribu kujitangaza kwa njia hii na kutengeneza hii kitu kwamba VICOBA wanaweza kukopa hadi Milioni kumi… kwanza mimi siwezi kukopa Milioni 10..“– Wema Sepetu.

0 comments :

Post a Comment